Recent comments

Fahamu Processor ni nini

Processor au CPU ndio ubongo wa kompyuta, kwa maana nyingine processor ndio inafanya kila kitu katika kompyuta kuanzia kupiga ziki, kuangalia picha, kuvinjari katika mtandao pamoja na kazi zote za kompyuta kwa kutumia mahesabu ya 0 na 1 kama tulivyoona katika bit. Wengine huwa wanachanganya CPU na lile jumba linalobeba kompyuta (Computer case).
Ndani ya processor kuna vitu vinavyoitwa Regista na Logical sakiti, sasa hizi regista ndizo zinazosaidia katika kutunza data za ndani ya processor wakati processor ikiendelea na mahesabu ili kufanya shughuli fulani ya kompyuta. Kwa hiyo kuna ukubwa wa regista katika mfumo wa processor wa 32-bit ni 32-bit na hivyo kwa 64-bit ni 64-bit. Kwa hiyo kinachofanya tupate aina hizi mbili za processor ni Regista zilizomo ndani yake.
Kwa hiyo unaona kabisa 64-bit processor inaipa uwezo kompyuta wa kufanya mambo makubwa kwa sababu ina hifadhi kubwa katika ubongo wake (CPU) ukilinganisha na 32-bit processor.
Fahamu Processor ni nini Fahamu Processor ni nini Reviewed by Positive thinking on 4:00 AM Rating: 5

3 comments

  1. Je inapokuwa imefeli kufanya kazi machine inakuaje inawaka au mana gafla lap top yangu haiwaki feni haizunguki

    ReplyDelete
  2. Na kama computer ina waka lakini kwenye monitor haionyeshi kitu chochote na ram pamoja na vja cable vipo vizuri tatizo linakua ni nini?

    ReplyDelete

Recent