Recent comments

VITU 10 VYA KUZINGATIA KABLA YA KUNUNUA LAPTOP

Kununua laptop inayofaa sio kitu rahisi kama wengine wanavyofikiria.....Kwani kuna vitu muhimu vya kuzingatia kama vile..Ukubwa,uwezo,utumiaji kwa urahisi n.k,Hivyo basi kuna vitu muhimu vya kuzingatia kwa mnunuzi wa laptop yeyote yule anahitaji kuzingatia yafuatayo. 

  • Processor,inachangia sana katika ufanisi wa kazi...hapa naongelea uwezo wa kuchanganua mambo yote yanayoendelea katika computer,kama unatumia computer kwa kazi fulani zinazotumia programs nzito kama vile Adobe designing programs,architecture programs,video productions programs unahitaji processor ambayo ni kubwa,mf,2GHZ,dual core,core i3,corei5,core i7. ila kwa matumizi ya kawaida kama masomo na shughuli za kawaida za kiofisi unahitaji processor yenye uwezo wa kawaida mf,1.8GHZ,dual core,core2duo,core 13 n.k

  • Battery,battery inakaa na chaji?kwa mtumiaji wa laptop katika nchi zetu zinazoendelea ambapo umeme wetu sio wa uhakika sana suala la battery pia ni la kulitazama
  • Nvidia display chip,kuna laptop nyingi zinazotumia graphic card ya NVIDIA zimekuwa zikisumbua na si tanzania tu bali dunia nzima,hivyo kwa kipindi hiki jaribu kuepuka laptop zenye sticker ya nvidia au angalia ndani kwenye upande wa device manager utaona nvidia video driver mf:hp pavilion na baadhi ya dell d620 na d630.chagua intel au ATI display card
  • Wireless hakikisha laptop unayonunua ina wireless kwani laptop za kipindi hiki nyingi zina wireless hivyo hata upatikanaji wa internet kupitia wireless ni mkubwa na urahisisha ufanisi na ni njia ya haraka pia
  • Ukubwa wa kioo,angalia ukubwa wa kioo cha laptop yako kwa mini laptop mara nyingi huwa ni 10.1 inch na kwa laptop za kawaida kwa sasa ni 15.4 na 15.6 inch,kati ya L:CD au LED ,epuka laptop zinazotumia display tofauti na hizo kama 13.3,17,18 inch kwani upatikanaji wake ni mgumu kwa hapa Tanzania na gharama huwa ni kubwa.
  • Harddisk,hii hutegemeana na mambo unayohifadhi kwenye laptop yako kama una vitu vingi itakubidi ununue laptop yenye harddisk kubwa mf,250GB,320GB,500GB,750GB n.k ila kama hauna mambo mengi unaweza nunua yenye uwezo mdogo tu kwani unaweza baadae unaweza nunua external harddisk
  • Memory/RAM,hii hutunza kumbukumbu ya programs unazozitumia ,ram hufanya kazi sambamba na processor katika kuhakikisha laptop yako inakuwa katika speed inayotakiwa,hivyo ram zinapokuwa kubwa na speed ya laptop inaongezeka ,standard kwa sasa ni kuanzia 2gb,4gb,8gb n.k
  • Operating system,kwa jina lingine tumezoea kuita window,hii ni program inayofanya kazi kwenye computer na kukusaidia wewe kutumia computer yako kwa urahisi,ni vyema kuchagua OS inayofaa kwa matumizi yako na pia iwe ya kisasa ili iweze kusapoti programs mbali mbali,
  • Uzito,angalia na matumizi yako na uangalie laptop ya kununua,kwani waweza kununua laptop kubwa mwisho wa siku ukashindwa hata kuibeba kwa urahisi au waweza kununua laptop ndogo ukashindwa hata kuona maandishi
  • warranty/guarantee hakikisha umepewa baada ya kununua laptop kwani muda mwingine unaweza kutana na laptop fake hivyo unaweza nunua baada ya mwezi tu ikafa,hakikisaha unapewa warranty au guarantee hata ya miezi 12 tu
  • VITU 10 VYA KUZINGATIA KABLA YA KUNUNUA LAPTOP VITU 10 VYA KUZINGATIA KABLA YA KUNUNUA LAPTOP Reviewed by Positive thinking on 4:03 AM Rating: 5

    5 comments

    Recent