Mambo 10 usiyoyafahamu kuhusiana na mfumo endeshi wa Android kutoka Google
Android ni mfumo endeshi unaotumika zaidi katika simu na tablets kwa sasa duniani kote kutokana na urahisi wake na wingi wa applications zinazoweza kutumika katika mfumo huo kutoka Play Store.
Mfumo endeshi huo kutoka Google kwa sasa umeliteka soko la mifumo endeshi ya simu na kuwaacha mbali sana wapinzani wake kama iOS, Windows, Blackberry na Symbian.Wengi tunaotumia vifaa vinavyotumia mfumo endeshi huu wa Google lakini kuna baadhi ya vitu hatuvifahamu kabisa. Hii ndo orodha ya mambo kumi ya kustaajabisha yanayohusiana na mfumo endeshi huu.1. Android haikugunduliwa na Google
Mfumo endeshi wa android uligunduliwa na Andy Rubin, Chris White, Nick Sears na Rich Miner kipindi hicho ikiwa inafahamika kama Android Inc mwaka 2013. Baadae Android ilinunuliwa na Google ambayo iliendelea kuumiliki mfumo endeshi huo mpaka sasa. Google walinunua mfumo endeshi huo kutoka kwa Android Inc August 2005 kwa dau la $50 milioni.
2. Google waliachia Android rasmi mwaka 2007
Mfumo endeshi wa Android uliachiwa rasmi na kampuni ya Google mwaka 2007 na kuanza kutumika katika smartphones na kamera. Hapo awali mfumo endeshi huo ulitengenezwa maalumu kwa ajili ya kamera.
3. Android ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya Kamera
Android kwa mara ya kwanza ilitengenezwa kwa ajili ya smartcameras, ila google waliona ubora wa mfumo endeshi huo katika simu na kuamua kuamishia katika simu na kuleta mapinduzi makubwa sana katika soko.
4. HTC Dream ni simu ya kwanza kuanza kutumia mfumo endeshi wa Android
Simu ya kwanza kuanza kutumia mfumo endeshi wa Android ilikuwa ni HTC Dream ambayo iliachiwa rasmi mwaka 2008 na kampuni ya HTC. Simu hiyo ilianza kwa kutumia toleo la android 1.0 na iliboreshwa mpaka kufikia toleo la android 1.6. Hapo mwanzo android ilipigwa madongo sana kuwa mfumo endeshi uliokosa mwingiliano mzuri na mtumiaji, japo baadae maoni hayo yalibadilika na kuiona android kama inaleta mapinduzi katika soko.
5. Android inatumika na zaidi ya watu bilioni moja duniani kote
Makamu wa Rais wa Google katika kitengo cha Android bwana Sundar Pichai, alitangaza kuwa kwa sasa mfumo endeshi wa android unatumika na zaidi ya vifaa bilioni 1 duniani kote katika nchi zaidi ya 190.
6. Majina ya matoleo ya Android yamekuwa yakipewa majina ya vyakula vyepesi au majina ya majangwa
Ukiacha android 1.0 na 1.1, matoleo mengine yote ya mfumo endeshi huu yamekuwa yakifuata majina ya vyakula vyepesi (sweet treats) au majangwa. Mfano wa majina hayo ni kama CupCake, Donut, Eclair, Froyo, Gingerbread, Honeycomb, Ice Cream Sandwich, Jelly Bean, Kitkat, Lollipop, Marshmallow na android N ambayo bado haijatoka rasmi.
7. Majina ya matoleo ya Android yanafuatana kwa Alphabets
Ukiangalia kwa makini majina ya matoleo ya mfumo endeshi huu utagundua yanafutana kwa alphabets.
8. Android ni Open Source (Huru na wazi)
Google wanatoa mfumo endeshi huu bure kwa watengenezaji na watumiaji wa mfumo endeshi huu na kuyapa nafasi makampuni mengi kutumia mfumo endeshi huo bila malipo. Hii inachangia sana kukua kwa mfumo endeshi huu.
9. Soko la wazi la kuuza na kusambaza Applications
Google ni mwanachama wa Open Handset Alliance (OHA), Android inawapa watumiaji wake ruhusa ya kutuia source code zake bure bila malipo. Hii imepelekea kuzuka kwa matoleo tofauti mengi ya Android ambayo hayahusiani moja kwa moja na Google.
10. Google inafaidika kwa kiasi kikubwa na Android
Kupitia matangazo katika baadhi ya app zinazouzwa katika Play Store, google inatengeneza kiasi kikubwa cha pesa kwa mwaka kuliko kampuni yoyote kwa sasa.
Mambo 10 usiyoyafahamu kuhusiana na mfumo endeshi wa Android kutoka Google
Reviewed by Positive thinking
on
3:02 AM
Rating:
No comments