Recent comments

VIPAJI NA NGUZO ZAKE KUPITIA FIKRA KATIKA UBONGO

1.   KIPAJI CHA UBUNIFU(INTROPERSONAL                                                            INTLLIGENCE)


Seli za fahamu zinatengeneza hali ya fikra zenye kina kikusanya mawazo pamoja kufanya maamuzi yenye mwelekeo uwezo wa kuchambuwa katika hali ya uhuru wa hiari.

Uwezo wa kujitathmini na kujifahamu kibinafsi kuanzia mawazo,hisia na utambuzi wa ndani.

Uwezo wa kuiongoza tabia binafsi, kujua nguvu na udhaifu, binafsi, kubuni fikra mpya,kupanga shughuli na kutatua matatizo.

MAENEO YA UFANISI WA KIPAJI

I.            Utambuzi wa viwango vya hisia binfsi.
II.            Uwezo wa kujitawa na kufanyia kazi mawazo na hisia binafsi.
III.            Njia nyepesi kueleza  mawazo  binafsi.
IV.            Hamasa ya kubaini na kutekeleza malengo.
V.            Ufanisi wa kazi uwapo huru mwenyew na peke yako.
VI.            Udadisi wa  kujuwa  maana ya maisha.
VII.            Kujitwala binafsi katika kujifunza kibinfsi na ukuaji.
VIII.            Kutamani sana kupata uzoefu wa ndani ya nafsi.
IX.            Uwezeshaji na uwamasishaji wengine.
X.            Kuja ukomo wa mipaka ya uwezo wako.

NAFASI ZA KITAALUMA.

a)   Jaji
b)  Mshauri
c)    Wakili
d)  Mwanasheria
e)   Mtaalamu wa matibabu.
f)     Mwndishi wa riwaya
g)   Mwana falsafa
h)  Mzee
i)      Kiongozi mwonaji

2.   KIPAJI CHA MAHUSIANO(INTERPERSONAL INTELLIGENCE)

NGUVU NA PEKEE WA KIPAJI

Seli za neva kutengeneza mawasiliano na wengine.

Mwingiliano wa kijamii, usikivu, ushirikishaji,kujenga mahusiano, utoaji na uwezo wa kuelewa na kufanya kazi vizuri na watu.

Wepesi na ukaribu wa kuchukuliana na watu na ushiriki wa kihisia wa mambo wanayopitia pamoja na uwezo wa kutawala, kusulubisha, kuongoza, kuelekeza na kushauri wengine.

MAENEO YA UFANISI

I.            Nguvu za kuongoza
II.            Ufanisi katika kujenga mtandao na wengine.
III.            Uwezo wa kujadiliana kujenga hoja za utetezi na mzuri katika usuluishaji
IV.            Uwezo wa kunasa/ kushawishi  wengine
V.            Uwezo wa kuongelea na kupangilia mambo.
VI.            Kufurahia kuwa mlezi wa vipaji vya wengine.
VII.            Uwezo wa kutanguliza wengine
VIII.            Uwezo wa kuhisi na kutambua hisia, hulka, tabia,matarajio ya wengine.
IX.            Ufanisi katika kufanya kazi na kundi, juhudi za pamoja katika kikundi, utendaji wa pamoja.
X.            Uwezo wa kuunganisha watu wakawa pamoja.
XI.            Uwezo wa kujenga mahusiano ya kijamii ya kudumu.

NAFASI ZA KITAALUMA

a)   Mwanasiasa
b)  Kiongozi wa dini
c)    Muuzaji
d)  Mkufunzi
e)   Mshauri
f)     Mtaalamu wa sayansi ya jamii
g)   Msemaji/ mtaalamu wa lugha
h)  Mtaalamu wa kijamii
i)      Mtaalamu wa saiklojia
j)      Afisa maendeleo
k)   Mkurugenzi wa rasrimali watu
l)      Meneja
m)           Mhamasishaji

3.   KIPAJI CHA LUGHA(LINGUISTIC THINKING)

NGUVU NA UPEKEE WA KIPAJI

Seli za neva zinazojenga umahili wa lugha na umakini wa maana za maneno, sauti,mahadhi pamoja na matumizi tofauti ya lugha mbalimbali

Uwezo wa kufikiri kwa njia ya maneno na kutumia maneno kwa fasaha katika kuongea na  kuandika .

Mwepesi wa kujifunza mifumo na mitindo ya lugha na matumizi yake.

MAENEO YA UFANISI WA KIPAJI

I.            Huhitaji kujieleza kwa kuandika au kutumia maneno mengi.
II.            Hupenda kulumbana, kuhoji, kuburudisha na kuelekeza.
III.            Hupenda kuandika, kucheza na maneno,kusoma na kusimulia visa na hadithi.
IV.            Huwa na kiwango kizuri cha elimu ya jumla.
V.            Huuliza maswali mengi
VI.            Hupenda kuongoza / kushiriki katika mijadala.
VII.            Hupendelea mbao za kuandikia , vifaa vya kutunza maneno na vifaa vya kunakili maneno
VIII.            Utamkaji vizuri wa maneno
IX.            Kujifunza lugha kwa urahisi
X.            Huwa na kumbukumbu nzuri ya majina, tarehe na majina ya maneno

NAFASI ZA KITAALUMA

a)   Mhariri
b)  Mwandishi wa hotuba
c)    Mtunga mashahiri
d)  Mwandishi wa riwaya
e)   Mwanasiasa
f)     Mtunza hakimiliki
g)   Msemaji/ mtaalamu wa lugha
h)  Mwandishi wa michezo ya kuigiza
i)      Mwanasheria/ wakili
j)      Mwandishi habari
k)   Mkufunzi

4.   KIPAJI CHA HESABU(LOGICAL/MATHEMATICAL THINKING)

NGUVU NA UPEKEE WA KIPAJI

Seli za neva zinazojenga uwezo wa kufikiri na kuchambuwa mambo kisayansi.

Uwezo wa kuelewa kanuni na mifumo na michanganuo ya kimahesabu

Uwezo kutumia akili kuhesabu na kuchanganua matatizo ya kinadharia kwa kutumia mahesabu

MAENEO YA UFANISI WA KIPAJI

I.            Uwezo wa nidhamu ya ndani katika kufikiri
II.            Uwezo wa kuhesabu na kuthbitisha  majibu ya hesabu
III.            Uwezo wa kufikiria sana mambo
IV.            Shauku ya kujua nini kinafuata mbeleni
V.            Kupenda kutafakari mambo kimahesabu
VI.            Kupenda kubuni nadharia zinazoonesha jinsi kufanya mambo
VII.            Hupenda kuthibitisha usahihi wa kitu kabla ya kutumia
VIII.            Kuonesha uwezo wa kutumbua na kutatua matatizo

NAFASI ZA KITAALUMA

a)   Mwanasayasi
b)  Daktari wa tiba
c)    Mwanahisabati
d)  Meneja miradi
e)   Mhasibu
f)     Mkutubi wa chuo kikuu
g)   Mhandisi
h)  Mtafiti
i)      Mtaalamu wa program za kumpyuta
j)      Mataalamu wa tiba ya mifupa
k)   Mataalamu wa benki
l)      Mwanasheria
m)           Mpelelezi
n)  Mwindaji wanyama
o)  Mfanyabiashara/ mjasiriamali

5.   KIPAJI CHA MICHEZO(KINESTHETIC THINKING)

NGUVU NA PEKEE WA KIPAJI

Akili za miondoko, kugeuza maungo ya mwili na mizunguko hususani kucheza mpira wa miguu, riadha, kujitupa juu ya kiti bila kuanguka, kujigeuza mwili pasipo maumivu

Ufundi wa kutumia viungo vya mwili na miondoko na uwezo kumudu vitu au mambo yanayokuzunguka

Kuna baadhi watu walioumbwa kujifunza na kufikiria viwango vya ubora wa vipaji kwa njia ya michezo

MAENEO YA UFANISI WA KIPAJI

I.            Uwezo mzuri wa kujikusanya kimwili
II.            Mwepesi kuwahi muda na kufanya kwa wakati
III.            Hukabiliana na matatizo kwa nguvu za kimwili
IV.            Kupenda kunyoosha viungo vya mwili na mazoezi
V.            Kupenda michezo ya kuigiza
VI.            Kupenda kucheza ngoma/ muziki
VII.            Hufikiri wakati wa miondoko
VIII.            Hupenda kuchonga vinyago na burudani
IX.            Kubuni vitu vipya vya kimichezo

NAFASI ZA KITAALUMA

a)   Mwigizaji
b)  Mwanariadha
c)    Mcheza muziki
d)  Mvumbuzi
e)   Sonara
f)     Mchongaji
g)   Mwansanaa
h)  Mtaalamu wa umeme
i)      Daktari mpasuaji
j)      Dereva wa mashindano ya magari
k)   Mtaalamu wa tiba maungo

6.   KIPAJI CHA MZIKI(MUSICAL THINKINIG)

NGUVU NA UPEKEE WA KIPAJI

Seli za neva zenye uwezo wa kuimba au kupiga vyombo vya muziki, uwezo wa kuitambua mahadhi na kupambanua mambo yasiyo dhahiri kupitia muziki

Uwezo wa kuwasoma watu kwa kusikiliza sauti zao na lugha kuptitia maungo ya mwili na sio kwa kusikiliza maneno peke yake

Hutumia kwa  sehemu ya ubongo iitwayo sular ambayo fikira za muziki na hutumia utambuzi wa ndani wa kufahamu mambo yasiyo dhahiri.

MAENEO YA UFANISI WA KIPAJI

I.            Utambuzi wa ndani kuhisi wakati mambo ni mazuri au mabaya
II.            Hafanyi mambo mpaka amejisikia yuko sahihi
III.            Hawezi kujieleza lakini ni ana hisia za kutambua ni nani wa kuaminiwa na ambaye siye
IV.            Yuko makini  na hisia kali na mazingira na kujisikia au kutojisikia raha katika maeneo Fulani .
V.            Hutafuta kusikiliza sauti, huvutiwa na muziki na hupenda kutunga nyimbo/ muziki
VI.            Uwezo wa kuimba vizuri kwa vina na mjunzi wa kupiga vyombo
VII.            Uwezo wa kusikiliza na kukosoa muziki
VIII.            Ukusanyaji wa vyombo, ala na muziki
IX.            Hupenda kuchezesha miguu, vidole au kalamu anapofanya kazi au kusikiliza jambo.

NAFASI ZA KITAALUMA

a)   Mwongozaji
b)  Mtunga ala
c)    Mtunzi wa nyimbo
d)  Mhandishi wa muziki
e)   Mtaalamu wa kinanda
f)     Msimamizi wa disko
g)   Mwalimu wa muziki
h)  Mtaalamu wa nyimbo za ala
i)      Mchezaji wa jukwaa
j)      Mchezaji muziki
k)   Mwanamuziki
l)      Mwimbaji
m)           Mhandishi wa uzalishaji muziki
n)  Msemaji wa  Umma(MC)

7.   KIPAJI CHA PICHA(VISUAL/SPATIAL THINKING)

NGUVU NA PEKEE WA KIPAJI.

Seli za neva za kutazama rangi, mwanga,umbo na vina vya vitu, ikiwa ni pamoja na kufumba macho au kutafakari kuona mambo ambayo hayaonekani kwa macho asili.

Uwezo wa kukitoa kitu kwenye nafsi ya ndani (non-concious) hadi kwenye akili (consiousness).

Uwezo wa kupokea kutoka ulimwengu wa picha/maumbo na kutengeneza ramani za kiakili, hadi kutoa kitu halisi kwa mfano wa picha kutoka akilini.

MAENEO YA UFANISI WA KIPAJI

I.            Hufikiri katika mfumo wa picha kutafsiri michoro/ picha kwa urahisi
II.            Uwezo wa kupokea mawazo kwa njia ya maumbo na kuyachora mawazo hayo katika mfumo wa picha.
III.            Uwezo wa kukukumbuka sura lakini husahau majina
IV.            Huweza kufusha mawazo huku akiendelea kusikiliza
V.            Kuendesha kupitia na uwezo wa kupita kwa kwenye msongamano wa amgari barabarani/ mitaani

NAFASI ZA KITAALUMA

a)   Mmchongaji
b)  Mwanamazingira
c)    Kiongozi
d)  Mtendaji mkuu
e)   Mbunifu wa mchoro
f)     Mhandisi
g)   Mwandishi wa Sheria
h)  Nahodha
i)      Mtaalamu wa video
j)      Mpiga picha
k)   Mpiga picha ramani
l)      Mpaka rangi
m)           Mtaalamu wa jadi
n)  Mwendeshaji
o)  Msanifu wa majengo
Rubani
VIPAJI NA NGUZO ZAKE KUPITIA FIKRA KATIKA UBONGO VIPAJI NA NGUZO ZAKE KUPITIA FIKRA KATIKA UBONGO Reviewed by Positive thinking on 12:59 PM Rating: 5

1 comment

Recent