Cloud Computing na faida zake, Ubaya wake na Ushauri wake
Kwa
urahisi kabisa cloud computing ni kitendo cha kuhifadhi data au applications
zako kwenye server maili kadhaa kutoka ulipo wewe. Kila unapotaka kuzitumia
unaingia kwenye Internet na kuingia kwenye account yako na kuzikuta hapo.
Hakuna haja ya kuzihifadhi kwenye komputa yako, unakuwa unazipata na kuzitumia
pale unapozihitaji tu siyo tu kwa kutmia komputa bali kwa kutumia kifaa
chochote kama simu ya mkononi, tablets, notebook, n.k. Hii inamaanisha una
uwezo wa kuzitumia data zako wakati wowote na mahali popote ulipo. Watu
wengi na makampuni mengi yanajiingiza kwenye mfumo huu kwa sababu ya urahisi
wake. Kwa kutumia cloud computing hauhitaji tena komputa yenye storage capacitykubwa
sana nyumbani kwako, kumbuka data zako zinahifadhiwa mahali pengine kabisa. Hii
inaleta urahisi kwa sababu hununui komputa ya ghali sana. Pia kumbuka komputa
inatumia umeme hivyo unakuwa unatumia umeme mdogo zaidi kama uko kwenye cloud
ukilinganisha na mtu anayehifadhi kila kitu kwenye system yake nyumbani. Kwa
makampuni gharama za kununua hardware zinapungua sana.
Japokuwa
tunayazungumzia mazuri ya cloud computing, si kweli kwamba basi tusahau mfumo
tuliouzoea wa kuwa na komputa na kila kitu ndani yake nyumbani kwako. Ukweli ni
kwamba unahitaji Internet connection kila mara unapotaka kutumia data zako au
applications services. Hii ni mbaya hasa kwa nchi kama za kwetu Africa ambapo
kuna matatizo ya Internet na umeme. Tatizo lingine kubwa ni
data security. Wakati makampuni mengi yanayohifadhi data zetu kwenye serves zao
wanatuhakikishia kwamba watazihifadhi data zetu vizuri, usalama wake ni mdogo
kwa maana anayezihifadhi ni mtu mwingine na wala huwezi kugundua ikiwa
atazitumia au kuziangalia data hizo bila ruhusa yako. Hii ni hatari zaidi kwa
makampuni kwa maana siri zao za kibiashara zinakuwa zinahifadhiwa na mtu
mwingine mahali pengine.
Ushauri
Ni
vizuri kama tunataka mafanikio, kuhakikisha kabla ya kujiingiza kwenye
teknolojia hii, basi tunajua faida na madhara yake. Elimu ya teknolojia hii
itakusaidia kufahamu kama unahitaji cloud computing kwa matumizi yako au ya
biashara yako. Kuna wale wanaopendelea urahisi wa kuweza kuzi-access data zao
wakati wowote na mahali popote (flexibility and mobility) lakini wapo wale
wanaopendelea kuwa na uhakika kwa kuhifadhi data zao wenyewe (ownership and
control).
Cloud Computing na faida zake, Ubaya wake na Ushauri wake
Reviewed by Positive thinking
on
3:05 AM
Rating:
No comments