Sababu zinazofanya komputa iwe slow
1. Background Programs : Inawezekana kila unapowasha komputa yako kuna background programs usizozihitaji kwa wakati huo zinaanza kufanya kazi bila wewe kujua. Yawezekana ni programs genuine au spyware.
a. Kuziona na Kuzifunga programs hizi bonyeza Ctrl +Alt + Delete kwa wakati mmoja.
b. Bonyeza ‘Start task manager’
c. Bonyeza ‘Processes’
d. Zianzoonekana ni processes zinazofanya kazi kwa wakati huo. Unaweza ukaanza kuondoa moja baada ya nyingine kwa kuchagua process unayotaka kutoa na kubonyeza ‘End task’. Jaribu kutokutoa process muhimu zinazosaidia System yako kufanya kazi. Hizi process ni kama Explorer na Systray
Kumbuka process hizi zitarudi next time utakapowasha tena komputa yako. Kama unataka zisiwe active kabisa basi nenda kwenye faili zilipohifadhiwa kisha configure kwa kuzi-disable.
2. Hard Disk : Inawezekana hard disk ya komputa yako ina data nyingi mno ambazo hazijajipanga vizuri hivyo kuifanya iwe slow. Ili hard disk ifanye kazi vizuri inahita free space ya 300MB – 500MBs. Hakikisha unafuta mafaili usiyohitaji. Sababu nyingine inawezekana hard disk yako iko fragmented kitu kinachosababisha programs kuwa loaded na kuwa deleted kila mara. Hakikisha una-run Windows hard disk defragmenter (Defrag) angalau mara moja kila mwezi.
3. Memory : Hakikisha una memory capacity ya kutosha. Kumbuka programs kama video na komputa games zinahitaji memory capacity kubwa zaidi. Jua matumizi ya komputa yako kabla hujanunua ili kuhakikisha unanunua komouta yenye memory capacity itakayokidhi mahitaji hayo. Kwa programs nyingi za kisasa hakikisha una angalau memory capacity ya 256 MB.
4. Windows Devices: Wakati mwingine kama umefanya madiliko fulani kwenye komputa yako, inawezekana kukawa na Windows device drive conflicts. Kwa mfano inawezekana una video drives mbili zinazoshindana. Kuondoa hili tatizo washa komputa yako kwenye Safe Mode kwa kushikilia F8 button wakati unapoiwasha komputa. Wakati uko kweny Safe Mode, bonyeza Start/Settings/Control Pane/System/Devices Angalia kila device kuhakikisha kama kuna yeyote yenye alama ya njano (warning sign) au alama nyekundu inayomaanisha kwamba kuna conflict kati ya drives. Cha kufanya hapa ni kuiondoa kabisa drive hiyo na kui-install nyingine upya.
5. Deleted programs : Baadhi ya programs ulizofuta zimeacha vichembe kwenye komputa yako. Tumia programs kama registry au PC cleaner kusafisha memory na registry.
6. Spyware au Adware : Inawezekana komputa yako imejaa spyware au adware programs zinazoiba data zako na kufanya vitu usivoyvihitaji na vingine ambavyo ni hatari. Tumia Ant-Virus programs kuhakikisha unajikinga na wadudu hawa.
Program ziifuatazo zitakusaidia kuichunguza system yako na kuondoa uchafu wote usiohitajika. Ni za bure kabisa hivyo usilipe chochote. Kwa wale wanaotaka program za kulipia zenye features nyingi na advanced zaidi basi bonyeza hapa.
Sababu zinazofanya komputa iwe slow
Reviewed by Positive thinking
on
3:11 AM
Rating:
No comments