UTAFITI: Manyanyaso kwa mtoto husababisha kubalehe mapema
Wataalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha
Penn State, Marekani wamegundua katika utafiti wao kuwa zaidi ya 90% ya watoto
waliopitia maisha ya kunyanyaswa, kupigwa au kudhalilishwa kingono wanabalehe
haraka ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa upendo.
Professor Jennie
Noll aliliambia
Jarida la Adolescent Health: >>> “Watoto hasa wa kike wanaolelewa kwa kunyanyawa hasa kupigwa
au kubakwa hubalehe kabla ya muda ukilinganisha na watoto wanaolelewa kwa
upendo pia watoto wa aina hii huota matiti mapema ukilinganisha na watoto wa
kawaida.“
Akielezea uhusiano ulipo baina ya mtoto
kunyanyaswa na kubalehe kabla ya wakati Dr. Noll alisema watoto wanaokuwa
katika mazingira kama hayo huzalisha homoni nyingi zinazotokana na msongo
mkubwa wa mawazo hivyo kuharakisha muda wa balehe. Wanasaikolojia hao
pia walisema mtoto anayenyanyaswa yuko hatarini zaidi kupata saratani ya ovari
na matiti ukilinganisha na watoto ambao hulelewa kwenye mazingira ya upendo na
amani.
UTAFITI: Manyanyaso kwa mtoto husababisha kubalehe mapema
Reviewed by Positive thinking
on
2:32 AM
Rating:
No comments