YAFAHAMU MAFUNDISHO YA UONGO
YAFAHAMU
MAFUNDISHO YA UONGO
(basi roho
anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani
wakiyasikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya shetani……wakiwazuia watu wa
sioe na……1Timotheo4:1-5)
SABABU ZA
MSINGI ZA KUYAFAHAMU MFUNDISHO YA UONGO
1. Ili tusiwe na kuishindania imani
ambayo watakatifu wamepewa mara moja tu (Yuda1:3)
2. Ili tuweze kuvipiga vita vizuri vya
imani na kuilinda imani mpka wakati tutakapomaliza mwendo ulioko mbele yetu
(2Timotheo4:7)
3. Ili tusiwe watoto wachanga na kutupwa
kule na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu za kigeni na mafundisho ya kishetani
(Efeso4:14)
4. Ili tusichukuliwe na mafundisho ya
kigeni yaliyo na mapokeo ya wanadamu na mafundisho ya shetani (Waebrania13:9 ,1Timotheo4:1)
MAFUNDISHO YA
UONGO NI YAPI?
Lolote
lililo kinyume na kweli ya Mungu yaani biblia linatokana kwa Baba wa uongo
ambaye ni Ibilisi (SHETANI). Kwa hiyo , tunatakiwa kuelewa kuwa shetani ni Baba
wa uongo na kwake kamwe haitoki kweli bali ni uongo(Yohana8:44) Kwa hiyo ili
shetani afanikiwe kupata watu atakaokwenda nao motoni yaani Jehanamu yeye
shetani amebuni ya kuwaletea mafundisho ya uongo yaliyo nje ya kweli
Mung(Wakolosai2:8)
JE! UTAJUAJE
KUWA HAYA NI MAFUNDISHO YA UONGO?
Kwa hiyo
tutaweza kufahamu kuwa haya ni mafundisho ya uongo ni kupitia neon la Mungu
(BIBLIA) , lolote lilo kinyume na neno
la Mungu latoka kwa Shetani. Hivyo tukitafuta kutoka katika kitabu cha Bwana
(BIBLIA) kwa njia ya kufundishwa mafundisho kama hivi tutaweza kuyafahamu
mafundisho ya uongo (Isaya34:16)
Kwa sababu
ya kutokuwa tayari kufundishwa ndiyo maana wengi wamejikuta wakiingia katika
mafundisho ya neno la Mungu. Hivyo tutafute kujifunza toka katika neno la Mungu
sio hadithi za wazee na za uongo miyume na watakatifu waliotangulia
hawakutafuta kweli toka katika hadithi za wanadamu zilizotungwa (2Petro1:16 ,
2Petro2:1-3 ,Wakolosai2:8 ,Efeso5:6-8 ,Marko7:6-8,13). Kwa hiyo tukitaka
kuyafahamu mapenzi ya Mungu katika kila jambo lazima tuyachunguze maandiko
matakatifu (BIBLIA) inasema nini na wala sio hadithi za wazee (Matendo17:11 ,
Mathayo22:29 ,Zaburi119:105)
YAFAHAMU
MAFUNDISHO YA UONGO
Baada ya
kuokoka ni vizuri kuyaahamu mafundisho ya uongo na mashetani ili upate kuitetea
imani yako na kulinda wokovu wako ulioupokea kutoka kwa YESU KRISTO.
A. KUWAZUIA WATU WASIOE (1Timotheo4:1-3)
Kwa hiyo hakuna mahali popote katika biblia ambapo watu
Wamezaliwa wasioe, ila tunaona Mungu ametoa agizo la watu kuoa ili wapate
kuijaza nchi (Mwanzo2:18-24, Mwanzo1:27-28). Mtume Paulo alisema mtu akiweza
kukaa kama yeye kwa ajili ya Bwana Yesu ni vema , lakini haikuwa na maana
aliwazuia watu wasioe (1Wakorintho7:8-9) kwa hiyo moja ya sifa zaa msingi kwa kiongozi wa kanisa ni kuona kwa hiyo
nizuri wachungaji ,makasisi , mapadri , wazee/walehi , mashemasi
na wengineo wakaoa (1 Timotheo3:1-2
B.
KUABUDU SANAMU
(Kutoka20:4-5)
Kwa hiyo kuabudu sanamu ni moja mafundisho ya uongo nay a
kishetani ambayo sisi kama watoto wa Mungu tunatakiwa kuwa mbali sana mahali
wanapofundisha mafundisho hayo(WAlawi26:1 , Kumbukumbu4:16-19 , Isaya31:7-1 ,
Wakorintho10:14-22 , Yohana5:21)
C.
KUPINGA WOKOVU(Marko16:15-16,
mathayo28:19-20)
Mojawapo ya
mafundisho ya uongo ni kupinga kuwa hakunakuokoka yaani wokovu na kwamba
kuokoka ni kule Mbinguni(Waebrania9:27 , Yohana3:16 , 1Timotheo1:15 , Warumi10:9-10,13)
D. KUBATIZA WATOTO WADOGO NA WALE WASIOAMINI (Mathayo10:14-16)
Kubatiza
watoto wadogo ni moja ya mafundisho ya uongo ya shetani kwa sababu hata Bwana
Yesu Kristo mwenyewe hakuagiza tubatize watoto wadogo ila alisema watoto wadogo
kama hawa ufalme wa Mbinguni ni wao hivyo Yesu aliagiza watoto wadogo
wabarikiwe na kuwekwa wakfu kwa bwana mbele ya madhabahu ya Mungu(Luka2:27-34)
E.
KUOMBA WAKFU NA KUENDESHA
IBADA KWA AJILI YA WAFU (Kumbukumbu18:9-12 , Kumbukumbu14:1-2)
Mafundisho
ya kuomba wafu na kuendesha ibada kwa ajili ya wafu ni mafundisho ya uongo nan
i mafundisho ya kishetani (Kumbukumbu14:12)
F.
HADITHI ZA KIZEE
(2Petro1:16 , 2Petro2:1-3)
Kwa hiyo
kuomba kupitia rozali , maji ya Baraka ni mafundisho ya mashetani na hadithi
zakizee. Hakuna mahali popote ndani ya biblia inaposema tuombe kupitia rozali
ila hiyo hadithi ni mawazo ya mtu
aliyeota ndoto na sio neno la Mungu
YAFAHAMU MAFUNDISHO YA UONGO
Reviewed by Positive thinking
on
2:30 PM
Rating:
Nafikiri mafundisho kwenye Biblia kadri ya nukuu sio ya uongo bali tafasiri ndizo za uongo.nilipofungua ambatanisho hili nikakutana na kichwa cha habari "yafahamu mafundisho ya uongo" nilitegemea kuyaona hayo mafundisho ya uongo badala yake nakutana na mafungu ya biblia yenye mafundisho sahihi.ukianza kutaja hayo mafundisho ndipo ufanye reference kwa kutumia hivyo vitabu utakuwa umetusaidia sana wasomaji dhidi ya mkanganyo.asante
ReplyDelete