Recent comments

Fahamu jinsi ya kurudisha kazi iliyopotea katika Ms Office


Nadhani hata wewe ulishawahi kukutwa na aina hii ya fedheha na ukashindwa kujua nini cha kufanya. Ondoa shaka leo nitakuelekeza jinsi ya kurudisha kazi yako uliyoifunga kwa bahati mbaya au kwa sababu ya kukatika kwa umeme katika Microsoft Word, Microsoft Publisher, Microsoft Excell pamoja na Microsoft Power Point. Njia hii inafanya kazi vizuri zaidi kwa vifurushi (packages) za Microsoft Office 2010,2013  na 2016 kwa sababu kazi unayoichapa huwa inahifadhiwa kwenye draft bila ya wewe kujua. Unaweza ukaset muda wa kazi kuwa saved automatically katika Tab ya save, ila kwa kawaida huwa inakuwa ni dakika 10.

  • Fungua Microsoft Office uliyokuwa ukitumia kama ni Word, Excel, Publisher au Power point
  • Bonyeza File Tab, upande wa kushoto juu kabisa, kisha bonyeza Recent
  • Bonyeza Recover Unsaved Document kama upo kwenye Ms Word, na Recover Unsaved Workbookkama upo kwenye Excel na Recover Unsaved Presentation kama upo kwenye power point.
  • Kazi yako iliyohifadhiwa kwenye draft itaonekana na utaifungua ili kuendelea kuiedit (kuifanyia kazi)
  • Baada ya kuifungua sasa kumbuka kuisave ili kupunguza uwezekano wa kuipoteza tena pale umeme unapokatika.
  • Fahamu jinsi ya kurudisha kazi iliyopotea katika Ms Office Fahamu jinsi ya kurudisha kazi iliyopotea katika Ms Office Reviewed by Positive thinking on 2:02 AM Rating: 5

    No comments

    Recent