Recent comments

Jinsi ya kupata mawimbi makali ya Wifi ofisini kwako au nyumbani kwako

Huwezi kupata Wifi kama huna kifaa kinachorusha mawimbi haya, Router au maarufu kama Wireless Router ndio kifaa kinachotumika zaidi katika kazi hii. Ubora wa kifaa chako ni sababu ya kwanza kubwa katika kuhakikisha unapata mawimbi ya kutosha. Unapoenda kununua router ni vizuri kununua inayoendana na mahitaji yako na idadi ya vifaa unavyotaka kuviunga.



  • Eneo sahihi la kuweka router yako ni katikati ya ofisi au jengo ili mawimbi yaweze kusafiri pande zote za chumba au nyumba kiurahisi bila kikwazo chochote.
  • Epuka kuweka router kwenye pembe za kuta au pembezoni mwa chumba au nyumba kwa sababu sehemu kubwa ya mawimbi yatatoka nje kwa majirani zako
  • Kumbuka vitu vigumu kama ukuta au mbao zinazuia mawimbi ya Wifi, hilo ni jambo la msingi kuzingatia unapoamua kuweka router yako
  • Usisahau kunyanyua au kuchomoa Wifi Antena katika router au kifaa chako, kama inazo sababu zina effect kubwa sana katika kutoa mawimbi makali ya Wifi na yanayosafiri umbali mrefu.
  • Epuka kuweka Microwave karibu na router sababu Microwave ni adui mkubwa sana wa mawimbi ya radio (radio signals) yanayotumika na router kusafirisha data. Ukitaka kujaribu uadui wa microwave na mawimbi ya radio jaribu kuweka simu yako karibu na microwave iliyowashwa, utaona inapoteza mtandao au inakuwa haina mtandao wa kutosha (Signal Jammer).
  • Chagua mtoa huduma za mtandao (ISP) anayeaminika katika eneo lako ili kuepuka usumbufu wa kukatika kwa signal kila wakati.
  • Chagua kifurushi chenye bandwidth ya kutosha kulingana na idadi ya watumiaji wako pamoja na aina ya shughuli unayofanya.
  • Kumbuka kurestart router yako kila baada ya muda fulani ili kuipa nguvu mpya ya kurusha mawimbi.
  • Update router firmware pale tu inpotoka firmware mpya ili kuongeza ufanisi
  • Disconnet vifaa vyote ambavyo havitumiki tena na Router husika, kama kopyuta zilizokufa au kuharibika.
  • Install application itakayokusaidia kukagua matumizi ya data na ukali wa mawimbi (signal strenght) katika kompyuta yako ili kukupa picha nzima ya kiasi cha data kinachotumika katika network yako.
  • Weka wifi password ngumu ili kupunguza wezi wa wifi yako.
  • Monitor application zote zinazotumia bandwidth kubwa katika kompyuta zako
  • Jinsi ya kupata mawimbi makali ya Wifi ofisini kwako au nyumbani kwako Jinsi ya kupata mawimbi makali ya Wifi ofisini kwako au nyumbani kwako Reviewed by Positive thinking on 2:02 AM Rating: 5

    No comments

    Recent