Recent comments

Jinsi ya kuweka bold na italiki katika WhatsApp


Watu wengi husumbuka sana wanapoandika ujumbe kwenye mtandao wa WhatsApp kutokana na hali kwamba herufi huwa na uzito sawa wa rangi katika hali ya kawaida. Hi indo njia itakayokufanya uweza kukoleza rangi ya herufi na kuzifanya nzito (bold), ukaziweka kwa mlazo (italiki) na pia ukaweka mstari unaozikata herufi kati, kwa Kiingereza strikethrough Unachohitaji kufanya kwanza kabisa ni kuwa na toleo la karibuni zaidi la app ya WhatsApp kwenye simu yako.

Je, wajua unaweza kukoleza rangi ya herufi na kuzifanya nzito (bold), ukaziweka kwa mlazo (italiki) na pia ukaweka mstari unaozikata herufi kati, kwa Kiingereza strikethrough?
Unachohitaji kufanya kwanza kabisa ni kuwa na toleo la karibuni zaidi la app ya WhatsApp kwenye simu yako.

Kuweka bold

Ili kukoza rangi kwenye herufi (kufanya bold), unahitajika kutanguliza neno lako na alama ya nyota na kisha kuhitimisha na alama ya hiyo hiyo nyota.
Kwa mfano, ukiandika *bold* itatokea ikiwa bold

Kuweka italiki

Ili kufanya herufi zako kuwa za mlazo au kuwa za italiki, unahitajika kutanguliza na mstari sakafu (underscore) na kuhitimisha na alama iyo hiyo.
Ukiandika _italics_ itatokea ikiwa italics

Kuweka strikethrough

Ukitaka kuweka alama ya kukata kati kwenye herufi zako, unahitajika kuanza na alama ya mawimbi au kwa Kiingereza tilde (~) na kuhitimisha na alama iyo hiyo.
Ukiandika ~strikethrough~ itatokea ikiwa na mstari uliokata herufi kati.

Kuunganisha mitindo

Unaweza ukataka kuunganisha mitindo, mfano utake kuwa na bold na italiki.
Utahitajika kutumia alama za unachohitaji katika kuanza neno lako na kuhitimisha.
Mfano, ukiandika _*bolditalics*_ inafaa kutokea ikiwa bolditalics.
Image 
Jinsi ya kuweka bold na italiki katika WhatsApp Jinsi ya kuweka bold na italiki katika WhatsApp Reviewed by Positive thinking on 1:41 AM Rating: 5

No comments

Recent