Jifunze jinsi ya ‘kufollow’ watu wote ‘uliounfollow’ kwa pamoja katika Facebook
Kuna muda hupendi ukurasa wako wa facebook kujaa habari, taarifa na picha zisizo na maana. Unaamua kufuta watu au kurasa zote zinazotuma habari au picha usizozipendelea mara kwa mara katika ukurasa wako. Muda mwingine hujisikii kupokea post kutoka kwa baadhi ya watu kabisa.
Kuna wakati pia unajikuta ukiwa na uhitaji wa kurudisha watu au kurasa ulizocha kuzifuata (follow) kwa dhumuni maalumu. Sasa hapa ndipo kazi inapokuja, kwa hali ya kawaida utahitajika kutembelea kila kurasa ya page unayotaka ili uweze kuifuata tena (follow). Sasa fikiria kama kurasa ulizofuta zinafika 200, hapo shughuli inakuwa kubwa zaidi.
Facebook wameliona hilo na wamekuwekea uwezo wa kuweza kufuata kurasa au watu wote uliocha kuwafuata (unfollow) kwa pamoja.
Kufuata watu wote uliocha kuwafuata kwa pamoja kwa kutumia kompyuta (Following all unfollowed people on desktop)
- Ingia kwenye ukurasa wako wa Facebook.
- Nenda mpaka upande wa kushoto wa ukurasa wako wa Facebook na tafuta sehemu iliyoandikwa News Feed.
- Ukiweka kasa hapo, kuna kialama cha rangi ya kijivu inaonekana katika sehemu hiyo kikiwa na umbo la gia ikimaanisha mipangilio (settings), bonyeza hapo.
- Bonyeza Edit Preferences
- Bonyeza Reconnect with people you unfollowed, itafungua orodha ya watu au kurasa na makundi yote uliacha kuyafuata, hapo utachagua yale makundi, kurasa au watu unaotaka kuwafuata tena na kuacha wale usiowataka. Unaweza ukachuja matokeo kwa watu, kurasa au makundi.
- Baada ya hapo bonyeza Done kuhifadhi mipangilio (save settings).
Kufuata watu wote uliocha kuwafuata kwa pamoja kwa kutumia simu (Following all unfollowed people on Mobile App)
- Katika App ya Facebook gusa sehemu ya mipangilio (settings)
- Shusha chini na chagua News Feed Preferences.
- Gusa kwenye Reconnect with people you unfollowed.
- Gusa kwenye picha kuchagua watu, kurasa au kundi unalotaka kulifuata tena.
Taarifa na vitu vinavyopostiwa na watu hawa vitaanza kuonekana tena katika ukurasa wako. Hii inapunguza muda kutembelea ukurasa mmoja mmoja wa kila mtu na kuanza kumfuata tena.
Jifunze jinsi ya ‘kufollow’ watu wote ‘uliounfollow’ kwa pamoja katika Facebook
Reviewed by Positive thinking
on
2:06 AM
Rating:
No comments