sehemu salama ya kupata softwares za bure za Windows
Ninite.com
ni sehemu pekee unayoweza kudownload na kuinstal software za Windows bure na
kwa usalama zaidi kwa pamoja. Utofauti wa ninite.com ni uwezo wa kudownload na
kuinstal software nyingi kwa wakati mmoja yenyewe bila kumsumbua mtumiaji wa Pc
kuclick Next, Next… unapobadilisha Windows au tunapohamia toleo
jingine la Windows (Upgrade) huwa tunapata tabu sana katika kutafuta installer
za software zote za msingi kama Google Chrome, Adobe reader, Skype, Mozila
Firefox, VLC media player na kuziinstall mojamoja mpaka tunaporidhika. Kwa
kompyuta moja inaweza isiwe shida sana lakini ni tofauti kama una kompyuta
zaidi ya moja, kuzidownload na kubonyeza Next, next… ni jambo la kuchosha
kidogo. Hapa ndipo ninite.com inapoingia, ninite
itakusaidia kuinstall application zote za muhimu bila tabu wala usumbufu wowote
ule. Katika mtandao (tovuti) ya ninite utaona maelekezo jinsi kuinstal
application unazotaka, hakuna kitu kigumu zaidi ya kuchagua application au
software unazotaka na kuinstall bila tabu. Ninite yenyewe haitachagua offer au
tools bars zinazokuja na baadhi ya installer hivyo kukupa usalama zaidi.
sehemu salama ya kupata softwares za bure za Windows
Reviewed by Positive thinking
on
3:07 AM
Rating:
No comments