Recent comments

Jinsi Virusi vinavyo shambulia Komputa

Hapa inategemea sana na aina ya virusi aliyeingia katika kompyuta yako na lengo la tengenezaji wa hivyo virusi katika kufanikisha lengo analotaka. Kulingana na aina ya mashambulizi na madhara wanayoleta virusi hawa wamegawanywa katika makundi tofauti tofauti kama Virus, Spyware, Worms, Trojans na Adwares.
Virus wao wanafanya kama jina lao linavyoelekeza, kama walivyo virusi wa wanyama na virusi hivi vya kompyuta vinadhorotesha utendaji wa kompyuta yako kwa kufuta baadhi ya mafaili ya programu au data katika kompyuta yako. 
Spyware ni aina ya virusi vya kompyuta vinatengenezwa kwa lengo la kuiba data za mtumiaji wa komyuta. Mara nyingi spyware zinajihusisha na masuala kama ya kuiba passwords, pin na baadhi ya mafaili waliyoelekezwa.
Worms kwa lugha ya kiswahili ni minyoo, kama ilivyo minyoo ya binadamu worms wanatekeleza mashambulizi yao katika kompyuta kwa kujiongeza na kujaza nafasi ya kompyuta bila mtumiaji wake kufahamu
Trojans wao ni kama virusi wanaotumwa kufungulia mlango mashambulizi mengine. Mara nyingi trojans wanaingia wakiwa katika baadhi ya software au viambatanisho vya katika barua pepe tunazopakua kila siku mtandaoni.
Adwares hawa ni virus wa kompyuta wenye lengo la kutangaza biashara za makampuni fulani na mara nyingi wanapatikana katika mitandao.
Jinsi Virusi vinavyo shambulia Komputa Jinsi Virusi vinavyo shambulia Komputa Reviewed by Positive thinking on 2:50 AM Rating: 5

No comments

Recent